Highlands FM

Wakulima wa pareto watahadharishwa kuepuka vishoka

4 December 2023, 17:32

Baadhi ya wakulima wakipokea msaada kutoka kampuni ya pareto{PCT}

Mikoa ya Mbeya na Songwe ndiyo wazalishaji wakuu wa pareto na wakulima wamepewa wito kuuza zao hilo kwa wanunuzi wenye uhakika.

Na Lameck Charles

Wakulima wa zao la pareto katika mikoa ya Mbeya na Songwe wametakiwa kuepuka walanguzi (vishoka) wanaonunua zao hilo kiholela  bila kufuata  kanuni za ubora unaotakiwa.

Rai hiyo imetolewa na afisa wa kampuni ya pareto (PCT) Mussa Malubalo wakati akitoa msaada wenye thamani ya shilingi milioni moja, ikiwamo mabati na saruji  kwa waumini wa kanisa katoliki kigango cha Usoha Muungano wilayani Mbeya.

Aidha Malubalo amewaomba wakulima kuiuzia maua kampuni hiyo  kwani imekuwa na utaratibu wa kurudisha kwa jamii ikisaidia kwenye nyanja tofauti kama afya, elimu na dini.

Sauti ya afisa wa kampuni pareto Mussa Malubalo
Baadhi ya wakulima walioudhuria kikao hicho kutoka mkoa wa mbeya na songwe .

Changamoto ya ubora wa maua ya pareto ni moja ya sababu  iliyowafanya na baadhi ya wakulima kulimbikiza ndani maua ya pareto hivyo basi wakulima wametakiwa kwenda kuyauza maua hayo kwenye vituo vya PCT.

Sauti ya afisa wa kampuni

Padri  Ambrose Mponzi Paroko  wa Parokia ya Irambo ameishukuru PCT kwa msaada wao walioutoa ili kuweza kusaidia ujenzi wa kanisa linaloendelea kujengwa kijiji cha usoha mungano.

Helmani  Mwaifanyi Ni chifu wa uhamasishaji wa zao la pareto nyanda za juu kusini amesisitiza wakulima kuendelea  kushirikiana na Kampuni ya PCT kwa lengo la kuongeza tija kwenye uzalishaji wa zao hilo.

Mhamasishaji wa zao la paleto

Kwa upande wake Diwani wa kata ya maendeleo Daniel Nyamwale  amesema zao la pareto ni zao rafiki kwa mkulima wa hali ya chini kwani halina kiangazi wala masika mkulima anaingiza kipato chake muda wowote.

Sauti ya Diwani wa kata ya maendeleo

Nao baadhi ya waumini kwa kanisa katoliki kigango cha Usoha muungano wameishukuru kampuni ya Pareto (PCT) na kuahidi kuwa wataendelea kushirikiana kwa lengo la kuleta tija ya uzalishaji kwa mkulima na mwekezaji.

Sauti za wananchi

Mikoa ya Mbeya na Songwe ni mikoa pekee inayoongoza kwa uzalishaji wa zao la kibiashara la pareto nchini Tanzania huku wawekezaji kutoka kampuni ya PCT wakihakikisha zao hilo linazalishwa kwa wingi na soko lake kuwa na uhakika.