Highlands FM

Highlands FM wanolewa matumizi ya teknolojia, maadili

27 April 2024, 16:39

Mhariri wa Radio Tadio Hilali Ruhundwa akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa Highlands FM. Picha na John Ilomo

Tadio imekuwa ikitoa mafunzo mara kwa mara kwa wafanyakazi wa redio wanachama wake na kwa sasa inatoa mafunzo ya utangazaji wa mtandaoni hususani matumizi ya mitandao ya kijamii na maadili ya uandishi wa habari.

Na John Ilomo

Mhariri wa Radio Tadio Bw. Hilali Ruhundwa  ametoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa redio Highlands FM kwa lengo la kuendana na kasi ya teknolojia ya kisasa pamoja na kuwakumbusha kuhusu  maadili ya uandishi wa habari na utangazaji.

Bw. Ruhundwa ametoa mafunzo hayo katika ofisi za Highlands FM zilizopo Jacaranda jijini Mbeya na kusema kuwa imekuwa kawaida kwa Tadio kutoa mafunzo kwa wanachanma wake, hasa katika kipindi hiki kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

Sauti ya mhariri wa Radio Tadio Hilali Ruhundwa
Baadhi ya wafanyakazi wa Highlands Fm Radio 92.5 Mbeya katika picha ya pamoja na mhariri wa Radio Tadio Hilali Ruhundwa (wa tatu kutoka kulia). Picha na John Ilomo

Kwa upande wa waandishi wa habari wa Highland FM wamesema kuwa mafunzo haya yamekuwa na tija kubwa kwani kuna baadhi ya vitu ambavyo walikuwa hawavifamu na kupitia mafunzo hayo wamepata kufahamu lakini pia wamepata kukumbushwa kuhusu miiko na maadili ya uandishi wa habari.

Sauti za waandishi wa habari

Tadio ambayo ni taasisi ya muunganiko wa redio za jamii nchini Tanzania, imekuwa  na kawaida ya kutoa  mafunzo kwa wanachama wake wote waliopo ndani ya nchi kupitia jukwaa lake la radiotadio kwa kila mwaka kwa lengo la kuwakumbusha  miiko ya utangazaji pamoja na uandishi wa habari pamoja na uandishi wa habari wa mtandaoni.