Highlands FM

DC Mbeya atoa onyo kali wanaotaka kuvuruga amani

4 November 2023, 10:14

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa ametoa angalizo kwa watu wanaotaka kuvuruga amani / picha na samweli mpogole

Mwandishi Samweli Mpogole

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa ametoa angalizo kwa watu wanaotaka kuvuruga amani iliyopo na kuwataka kuacha mara moja kwani Mbeya ni kitovu cha amani na biashara

Ameyazungumza hayo kwenye mahafali ya kuhitimu kwa mafunzo ya jeshi la akiba(Mgambo) yaliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba Jijini Mbeya ambapo ametahadharisha kuwa wanaodhani kuwa Mbeya ni kitovu cha vurugu kujitathimini kwani wakazi wa Mbeya hawatokuwa tayari kupoteza muda kuhatarisha amani iliyopo hivyo Serikali Ipo imara kulinda amani kwa maslahi ya wakazi wa Mbeya

Hata hivyo Malisa amezitaka taasisi za ulinzi Wilaya ya Mbeya kuwatumia vijana hao wanahitimu mafunzo hayo katika shughuli za ulinzi kwa kuwapatia ajira na kuacha kutumia Askari wasiokuwa na mafunzo katika taasisi zao.

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Beno Malisa kwenye mahafali ya kuhitimu kwa mafunzo ya jeshi la akiba(Mgambo)