Highlands FM

Uhaba wa wahudumu wa afya katika kijiji cha mtanila chunya ni kero kwa wananchi

20 September 2023, 13:09

Kwa mujibu wa sera ya maji ,Maji ni muhimu kwa viumbe vyote duniani, bila maji hakuna uhai. Aidha maji ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.Upatikanaji wa maji safi na salama kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na usafi wa mazingira ni muhimu katika kulinda afya za wananchi.

Wananchi wa Kijiji Cha mtanila wilayani chunya wakiwa kwenye mkutano wa hadhara : picha na Thobiasmgimwa

Na mwanaisha makumbuli

Baadhi ya wanawake wa kijiji cha Mtanila, kata ya Mtanila halmashauri ya wilaya ya Chunya wamesema kukosekana kwa maji kwenye kijiji chao kunakwamisha shughuli za uchumi kwa kuwa wanatumia muda mwingi kutafuta huduma hiyo badala ya kuzalisha mali.

Wakihojiwa na Highlands Fm, Radio wanawake hao wamesema wanalazimika kutembea umbali mrefu kutafuta maji badala ya kufanya shughuli za kiuchumi.

Katika hatua nyingine wameelezea changamoto nyingine inayowakabili kuwa ni uhaba wa wahudumu wa afya, hivyo kupelekea kukosa huduma bora za matibabu ikiwemo afya ya uzazi.

Baadhi ya wanawake wakielezea changamoto katika Kijiji Cha mtanila chunya

Mwenyekiti wa kijiji cha Mtanila, Davidi Eduward amekiri kuwepo kwa changamoto hizo, huku akielezea hatua za za awali zilizochukuliwa.

Mwenyekiti wa Kijiji mtanila Davidi Eduward
Wananchi wa Kijiji Cha mtanila

Naye diwani wa kata ya Mtanila, Nicksoni Mwankuga amesema kata yake ipo kwenye mpango wa kunufaika na ongezeko la wahudumu wa afya.

Diwani wa kata ya mtanila Nicksoni mwankuga

Akizungumzia changamoto ya uhaba wa maji, amesema kijiji hicho ni miongoni mwa vijiji vitakavyonufaika na mradi wa maji bwawa la Matwiga.

Diwani Nicksoni mwankuga
Mwenyekiti wa Kijiji Cha mtanila Davidi Eduward