Highlands FM

Serikali kushugulikia changamoto za viziwi

28 September 2023, 12:56

Mratibu wa Huduma za ustawi wa jamii wizara ya afya Dibogo Raymond akizungumza na waandishi wa habari jijini mbeya ; Picha na Samwel Mpogole

Watu wenye uziwi wamekuwa wakipitia changamoto mbalimbali za kijamii hali inayopelekea kushindwa kufikia malengo yao

Na Samwel Mpogole

Wizara ya afya imesema kuwa inatambua changamoto zinazo wakabili walemavu hivyo inaendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha wanashughulikia kikamilifu.

Hayo yameelezwa na Dibogo Raymond Mratibu huduma za ustawi wa jamii wizara ya afya kitengo cha tiba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mbeya katika kuelekea kilele cha Cha maadhimisho ya wiki ya viziwi Duniani ambapo amesema Moja ya changamoto wanazoendelea kushughulikia ni pamoja na Usawa katika upatiwaji wa huduma za afya na miundombinu katika vituo vya afya na hospitali.

Mratibu ustawi wa jamii Dibogo Raymond

Sambamba na hayo Dibogo amewataka wananchi kuto wanyanyapaa watu wenye ulemavu bali kuishi kwa upendo na mshikamano kwani sote ni Ndugu.

Mratibu Dibogo Raymond
Picha na Samwel Mpogole