Highlands FM

Makanisa ya ufufuo na uzima yafungwa Mbeya

6 June 2025, 4:29 pm

Kanisa la ufuf na uzima likiwa limefungwa. picha na Mwandishi wetu

Makanisa sita ya Ufufuo na Uzima yafungwa Mbeya kufuatia agizo la serikali

Na Samwel Mpogole

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limefunga makanisa sita ya huduma ya Ufufuo na Uzima yaliyokuwa yakiendelea na shughuli zake kinyume na tamko la serikali lililotolewa Juni 2, 2025 kupitia Msajili wa Jumuiya za Kiraia nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Benjamin Kuzaga, amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la serikali linalozuia huduma zote za makanisa ya Ufufuo na Uzima kote nchini huku akisema makanisa yaliyofungwa ni yaliyopo  ZZK Mbalizi, Mtaa wa Mnadani Rujewa (Wilaya ya Mbarali), pamoja na wilaya za Chunya, Rungwe, Kyela, na Jiji la Mbeya.

Sauti ya SACP Benjamin Kuzaga

Kuzaga amesema kuwa Katika tukio jingine, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na maafisa kutoka Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za wizi na usafirishaji wa vyuma vya minara ya mawasiliano ya kampuni hiyo.

Sauti ya SACP Benjamin Kuzaga

Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kushirikiana katika kufichua vitendo vya uhalifu vinavyoathiri maendeleo ya sekta ya mawasiliano na usalama wa nchi kwa ujumla.