Highlands FM

Mvua zikielekea mwishoni TFS yaonya uchomaji misitu

6 June 2025, 10:00 am

Ridhiwani Gambalela. Picha na Samwel Mpogole

Jamii imeonywa kuacha uchomaji moto wa misitu kwa uzembe, kutokana na athari zake kwa uoto wa asili, makazi ya viumbe, na usalama wa binadamu

Na Samwel Mpogole

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imetoa onyo kali kwa wananchi kuacha mara moja tabia ya kuchoma moto katika maeneo ya misitu, hasa kipindi hiki ambapo msimu wa mvua unakaribia ukingoni.

Akizungumza na Highlands FM, Afisa Habari wa TFS wa Kanda hiyo, Bw. Ridhiwani Gambalela amesema vitendo vya uchomaji hovyo wa misitu vina athari kubwa kwa mazingira, ustawi wa jamii na hata uchumi wa taifa.

Sauti ya Ridhiwani Gambalela

Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wameeleza maoni yao kuhusu changamoto na ufahamu juu ya athari za uchomaji moto katika misitu.

Sauti ya wananchi

Katika hatua nyingine, Bw. Gambalela ametoa wito kwa Watanzania, hususan wakazi wa Nyanda za Juu Kusini, kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo katika maeneo yao. Amesema mikoa ya kanda hiyo imebarikiwa kuwa na mandhari ya kipekee na maeneo mengi ya kuvutia yenye historia, ikolojia na burudani ya aina yake.

Sauti ya Ridhiwani Gambalela

Amefafanua  kuwa utalii wa ndani siyo tu burudani na elimu kuhusu mazingira, bali pia unachangia kukuza uchumi wa jamii zinazozunguka vivutio hivyo na taifa kwa ujumla kupitia ajira, biashara ndogo ndogo na mapato ya serikali.