Highlands FM

Wananchi waipa heko tume ya ushundani {FCC} nyanda za juu kusini

9 July 2024, 17:17

Baadhi ya wananchi wilaya ya kyela wakipata elimu namna ya kutambua bidhaa feki

Na Lameck Charles

Highlands Fm Mbeya

Wananchi  wilayani kyela mkoani mbeya wameipongeza tume ya ushindani (FCC) Kanda ya nyanda za juu kusini kwa kuendelea kuwapa elimu  kuhusu haki za mlaji na viashiria vya   bidhaa bandia.

Wameyasema hayo kwenye maonesho ya biashara yafahamikayo kama Kyela Exbition yaliyofanyika kwenye viwanja wa kasumuu kyela.

Andason luiza ni Mkaguzi na ofisa toka tume ya ushindani amesema wananchi wameneshwa kushtushwa na uwapo wa bidhaa bandia mtaani huku wakishukuru tume hiyo kuwapa elimu itakayowasaidiam kufanya utambuzi wa bidhaa bandia.

Dicksn Mbanga ni mkuu wa kanda wa tume ya ushindani FCC nyanda za juu kusini amesema wametoa elimu kwenye viwanja hivyo vya kasumulu Kyela  ukizingatia eneo hilo lipo mpakani mwa  Tanzania na Malawi hivyo ni vyema wananchi wawe na uelewa kuhusu bidhaa bandia.