Highlands FM

Wananchi waishio mpakani waomba elimu zaidi chanjo ya polio

25 September 2023, 17:52

Mpaka wa Kasumulu wilayani Kyela mkoani Mbeya: Picha Samwel Mpogole

Baadhi ya wananchi waishio mipakani mwa Tanzania na Malawi wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu ya chanjo ya polio kwani baadhi yao wameshindwa kuwapeleka watoto wao kupata chanjo hiyo.

Na Samwel Mpogole

Wananchi waishio mpakani mwa Tanzania na Malawi wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu sambamba na utoaji wa chanjo ya polio kwani baadhi yao bado hawajafikiwa.

Wakiongea na kituo hiki kwa nyakati tofauti wananchi hao wameishukuru serikali kwa kuhakikisha inawafikia ambapo pia wametumia nafasi hiyo kuomba muda wa utolewaji chanjo uongezwe kwani kuna baadhi yao walikuwa mbali na maeneo yao ya makazi.

Sauti za wananchi wilayani Kyela

Josephine Manase

Chanjo ya polio ilianza kutolewa 21 September hadi 24 September kwa watoto wenye umri chini ya miaka 8 katika mikoa 6 ambayo  inapakana na nchi zenye mlipuko wa polio ambyo ni Rukwa, Kagera, Kigoma, Katavi,, Songwe na Mbeya.