Highlands FM

CCM yawaita wananchi kumpokea Dk.Tulia

10 November 2023, 14:14

Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho, taifa (NEC), Ndele Mwaselela : picha Lameck Charles

mwandishi lameck Charles

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya kimekamilisha maandalizi ya kumpokea Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini dokta Tulia Acksoni anayetarajia kuwasili kesho ikiwa ni siku chache tangu kiongozi huyo achaguliwe kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge duniani (IPU)

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu maandalizi hayo, Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho, taifa (NEC), Ndele Mwaselela ametoa shime kwa wananchi wote kujitokeza kesho jumamosi Novemba 11, mwaka huu kwenye viwanja vya Ruanda Nzovwe kwa ajili ya kumpokea kiongozi wao

Ndele Mwaselela

Aidha mjumbe huyo amejivunia nafasi aliyoishinda Dkt Tulia kwani kutokana na nafasi yake ya Rais wa mabunge duniani zipo fursa na mengi tutakayofaidika wanambeya na watanzania wote kwa ujuml

Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho, taifa (NEC), Ndele Mwaselela

Mwaselela amesema kwa kuwa ni mara ya kwanza kwa dokta Tulia kuwasili jimboni kwake tangu achaguliwe kuwa Rais wa umoja wa wabunge duniani, ni vyema wananchi bila kujali itikadi zao kujitokeza kwa wingi kwenye mapokezi hayo ya kihistoria.

Ndele Mwaselela

Ikumbukwe kuwa Dkt Tulia Akson ni Rais wa kwanza mwanamke kushinda nafasi hiyo ya Rais wa Mabunge duniani kwa bara la Afrika.