Highlands FM

Wananchi Mbeya watakiwa kutowanyanyapaa watu wenye ulemavu

1 December 2023, 15:54

Katibu tawala wa mkoa wa mbeya akizungumza na wananchi ambao walipata fursa ya kuudgulia maadhimisho hayo .Picha Lameck Charles

Watoto na watu wazima wenye ulemavu mara nyingi hukabiliwa na ubaguzi, unaosababisha kupungua kwa upatikanaji wa huduma za msingi za kijamii na kutotambuliwa kwa ujumla.

Na Lameck Charles

Jamii mkoani Mbeya imekumbushwa kuachana na tabia ya kuwanyanyapaa watu wenye ulemavu ikiwemo kuwafungia ndani, kwani kufanya hivyo kunafifisha malengo pamoja na ndoto za kundi hilo.

Msisitizo huo umetolewa wakati dunia ikiwa ikiwa inaelekea kuadhimisha siku ya walemavu ambayo itaadhimishwa Disemba 3, mwaka huu.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera ametoa rai hiyo kwenye maadhimisho ya siku walemavu  iliyoandaliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Child Support lenye makao makuu Iwambi jijini Mbeya.

Homera ambaye aliwakilishwa na katibu tawala wa wilaya ya Mbeya, Azizi Mohamed Fakili amesema ni lazima haki za watu wenye ulemavu zilindwe ili waweze kufikia malengo yao.

Sauti katibu tawala wilaya ya mbeya Azizi Mohamed

Katika hatua nyingine mwakilishi huyo wa mkuu wa mkoa amewapongeza wafanyakazi wa Shirika la Child Support Tanzania (CST) huku akiwasihi kuendelea kufanya kazi kwa moyo na kumuomba mkurugenzi wa )CST) Bi Noela Msuya kuongeza ufanisi  wa utoaji elimu kwa watoto wenye ulemavu  ikiwemo kuwafundisha kwa vitendo ikiwemo ushonaji,Ususi,Ujenzi.

Sauti katibu tawala wilaya ya mbeya

Akitoa taarifa mbele ya Mgeni Rasmi Maratibu wa Miradi wa (CST)Doreen Audax Mayani ameitaja miradi mbalimnbali inayoendeshwa na Shirika hilo hukua akiutaja mradi mpywa uatakao wanaufaisha wakazi wa mkoa wa Songwe,Rukwa na Katavi.

Sauti mratibu wa mradi Doreen Audax

Emanuel Mpelumbwe Akimwakilisha mkurugenzi wa Shirika (CST) ameiomba serikali kuboresha miundo mbinu kwa  shule za serikali kwa ajili ya watoto wenye ulemavu pamoja na ongezeko la waalimu wa elimu jumuishi.

Sauti mwakilishi wa mkurugenzi wa shirika la CST

Nao baadhi ya wazazi waliohudhuria hafla hiyo wamesema wanashukuru uwepo wa kituo cha (CST) kwani  wameona mabadiliko ya watoto wao tangu walipojiunga na kituo hicho na kuwataka wazazi walezi kuto watenga watu wenye ulemavu

Sauti Baadhi ya Wazazi

Maadhimisho ya watu wenye ulemavu mwaka huu yanatarajiwa kufanyika Kitaifa Makao mkuu ya nchi Dodoma huku kauli mbiu ikisema Tuungane kuokoa watu wenye ulemavu ili kufikia malengo endelevu.