Highlands FM
Highlands FM
3 November 2026, 4:00 pm

Kampeni ya Ongea na Kamanda jijini Mbeya imeongeza mwamko wa wanaume kuripoti vitendo vya ukatili vinavyofanywa na wake zao.
Na Mwanaisha Makumbuli
Kampeni ya Ongea na Kamanda inayoendelea jijini Mbeya imelenga kuifikia jamii moja kwa moja kwa ajili ya kutoa elimu na kupokea changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi, zikiwemo vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Akizungumza kuhusu utekelezaji wa kampeni hiyo, Mkaguzi wa Polisi Kata ya Igale, Kituo cha Polisi Mbalizi, Fatuma Ramadhani Bakari, amesema kupitia kampeni hiyo wamebaini mwamko unaoongezeka kwa wanaume kujitokeza kuripoti vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa na wake zao.
Sauti Fatuma
Amesema hali hiyo inaonesha umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili kuvunja dhana kuwa wanaume hawawezi kufanyiwa ukatili au kuripoti vitendo hivyo.
Aidha, amewataka wanawake kuepuka kuwafanyia ukatili waume zao, huku akiwahimiza wanaume kujitokeza kwa wingi kuripoti matukio ya ukatili wanayokumbana nayo ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
Sauti Wito kwa Wanawake