Highlands FM

Kituo cha ESRAC mbeya chasaidia kutambua watoto wenye mahitaji maalum

13 October 2026, 2:09 pm

Shule ya Msingi Mwenge{Picha na Thobias Mgimwa}

Kituo cha ESRAC kilichopo Mwenge, jijini Mbeya, kinaendelea kuwa msaada muhimu katika kutambua watoto wenye mahitaji maalum kupitia tathmini ya changamoto za ufahamu, usikivu na uoni.

Na Thobias Mgimwa

Kituo cha Tathmini, Rasilimali na Msaada wa Kielimu (ESRAC), kilichopo Mtaa wa Mwenge, Kata ya Luanda jijini Mbeya, kinaendelea kusaidia kutambua watoto wenye mahitaji maalum ili kuwaunganisha na huduma za elimu zinazolingana na mahitaji yao.

Kwa mujibu wa Afisa Elimu wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Andason Mwalongo, kituo hicho kilianzishwa mwaka 2014 na ni kituo pekee cha aina hiyo kinachomilikiwa na Serikali jijini humo.

Makala hii inaangazia umuhimu wa utambuzi wa mapema, ushuhuda wa wazazi walionufaika na huduma hizo, pamoja na mchango wa elimu jumuishi katika kuhakikisha kila mtoto anapata fursa sawa ya kujifunza na kuendeleza uwezo wake.

Sauti Makala na Thobias Mgimwa