Highlands FM

Mawakala wa mabasi kuchukuliwa hatua kwa kuzidisha abiria

20 November 2026, 9:52 am

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mbeya, SSP Notca Kilewa; Picha na Samwel Mpogole

Imekuwa kawaida madereva kuchukuliwa hatua kwa kosa la kuzidisha abiria, lakini sasa Polisi Mkoa wa Mbeya wameeleza kuwa mawakala wa mabasi nao watawajibishwa kwa kushiriki kupakia abiria kupita idadi inayoruhusiwa kisheria

Na Samwel Mpogole

Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mbeya, limeonya kuwachukulia hatua mawakala wa mabasi wanaohusika na upakiaji wa abiria kupita idadi inayoruhusiwa kisheria, badala ya kuwawajibisha madereva pekee.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mbeya, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP Notca Kilewa, amesema hayo wakati akizungumza na mawakala wa mabasi katika Kituo Kikuu cha Mabasi jijini Mbeya.

Sauti ya SSP Notca Kilewa

Kwa upande wake, Afisa Mfawidhi wa LATRA Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Shaban Mdende, ameeleza utaratibu wa utoaji wa leseni za muda kwa mabasi yanayohitaji kubadili njia katika kipindi hiki.

Sauti ya Eng. Shaban Mdende

Baadhi ya mawakala wa mabasi katika kituo hicho nao wametumia nafasi hiyo kutoa maoni yao

Sauti ya Jeremiah Morice ,Julius Kamwene na Rashid Simwanza – Mawakala
Mawakala; Picha na Samwel Mpogole