Highlands FM

Chunya yachukua hatua mapema kukabili El Niño

8 October 2026, 2:22 pm

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Tamim Kambona; Picha na Mwandishiwetu

Chunya yajipanga mapema kukabiliana na athari za mvua kubwa za El Niño, huku wananchi wakihimizwa kuchukua tahadhari.

Na Samwel Mpogole

Kukiwa na tahadhari ya uwezekano wa mvua kubwa za El Niño, Halmashauri ya Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya imeanza kuchukua hatua mapema, ikilenga kupunguza athari zinazoweza kujitokeza katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Maeneo yanayobainika kuwa katika hatari yameanza kufanyiwa maboresho, huku Halmashauri ikiendelea kuimarisha maandalizi ili kuhakikisha changamoto zinazoweza kusababishwa na mvua hizo zinadhibitiwa kabla hazijaleta madhara makubwa.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Tamim Kambona, anafafanua hatua zilizochukuliwa.

Sauti ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Tamim Kambona

Mbali na kuimarisha miundombinu na maeneo hatarishi, maandalizi yameelekezwa pia kwenye sekta ya afya, ambako Halmashauri inahakikisha wananchi watakaoweza kuathirika wanapata huduma kwa wakati.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Dkt. Zuberi Mzige, amesema dawa pamoja na mahitaji muhimu ya tiba yameandaliwa ili kukabiliana na mahitaji yatakayoweza kujitokeza.

Sauti ya Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Dkt. Zuberi Mzige

Hata hivyo, pamoja na maandalizi yanayofanywa na Halmashauri, wananchi nao wanahimizwa kuchukua tahadhari mapema, hasa wale wanaoishi katika maeneo yanayoweza kuathiriwa na mafuriko au athari nyingine za mvua kubwa.

Afisa Mazingira Wilaya ya Chunya, Raphael Mahimbo, anaeleza hatua ambazo wananchi wanapaswa kuzingatia.

Sauti ya Afisa Mazingira Wilaya ya Chunya, Raphael Mahimbo

Halmashauri ya Wilaya ya Chunya inaendelea kusisitiza umuhimu wa maandalizi ya mapema, huku wananchi wakitakiwa kufuatilia taarifa rasmi za hali ya hewa na kuchukua tahadhari kwa usalama wao na mali zao.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Dkt. Zuberi Mzige; Picha na Mwandishi wetu