Highlands FM

Tazara Mbeya SACCOS yawapa tumaini jipya watu wenye ulemavu

12 October 2026, 11:25 pm

Meneja wa Tazara Mbeya Saccos, Stanley Mgina; Picha na Samwel Mpogole

Kupitia mkopo wa Tumaini Jipya wenye riba ya asilimia 1, Tazara Mbeya SACCOS inalenga kuwafungulia watu wenye ulemavu milango ya fursa za kiuchumi na kujikwamua kimaisha

Na Samwel Mpogole

Chama cha Akiba na Mikopo cha TAZARA MBEYA SACCOS kimeanzisha mkopo wa Tumaini Jipya unaolenga kuwapa fursa zaidi watu wenye ulemavu kupata huduma za kifedha kwa riba ya asilimia moja, hatua inayolenga kuwawezesha kiuchumi na kuwafungulia fursa za maendeleo.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 33 wa chama hicho, Meneja wa TAZARA MBEYA SACCOS, Stanley Mgina, ameeleza utaratibu wa mkopo huo na namna unavyolenga kuwasaidia wanufaika.

Sauti ya Meneja wa Tazara Mbeya Saccos, Stanley Mgina

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa chama hicho, Seleman Gwimile, amesisitiza umuhimu wa kusimamia mipango ya chama ili kuhakikisha huduma za kifedha zinawafikia wanachama na makundi yanayohitaji fursa zaidi za kiuchumi.

Sauti ya Mwenyekiti wa chama hicho, Seleman Gwimile,

Baadhi ya wanachama wameeleza maoni yao kuhusu huduma za chama hicho na umuhimu wa kuendelea kuweka mifumo inayowezesha makundi mbalimbali kunufaika na huduma za kifedha.

Sauti ya baadhi ya wanachama

Kupitia mkopo wa Tumaini Jipya, TAZARA MBEYA SACCOS inalenga kupanua fursa za kifedha kwa watu wenye ulemavu na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi.