Highlands FM

Hatari ya ukatili wa kijinsia kupitia AI.

20 November 2026, 6:19 pm

Picha IA

Matumizi ya akili bandia (AI) kutengeneza picha na video za uongo zinazolenga kudhalilisha wanawake yameelezwa kuwa tishio kwa usalama, haki na utu wao, huku jamii ikihimizwa kuacha kusambaza maudhui hayo na kutumia teknolojia kwa uwajibikaji.

Na Mwanaisha Makumbuli

Matumizi ya teknolojia ya akili bandia (AI) katika kutengeneza picha na video za uongo zinazolenga kudhalilisha wanawake yameibua wasiwasi kuhusu usalama, haki na utu wa wanawake katika matumizi ya mitandao ya kijamii.

Teknolojia hiyo inayoweza kubadilisha sura, sauti au mwonekano wa mtu na kumuweka katika maudhui ya uongo, imekuwa ikitumika katika vitendo vya unyanyasaji wa kidijitali, ikiwemo kusambaza picha za uongo zenye maudhui ya kingono bila ridhaa ya wahusika.

ABASI MUSSA Mtaalamu wa mifumo ya computer anaeleza kuwa maendeleo ya AI yameongeza uwezo wa kutengeneza maudhui yanayofanana na uhalisia, hali inayoweza kufanya iwe vigumu kwa jamii kutofautisha picha au video halisi na zilizotengenezwa kwa teknolojia hiyo.

Sauti Mussa

JAMES SAMBUKA ni kutoa shirika la msaada wa kishria jijini mbeya anaitaka jamii kuacha kusambaza picha na video zinazodhalilisha watu, hata pale ambapo haijathibitishwa kuwa ni za kweli, wakieleza kuwa kusambaza maudhui hayo kunaweza kuongeza madhara kwa waathirika.

Sauti James

Wito umetolewa kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kutumia teknolojia kwa uwajibikaji, kulinda faragha za wengine na kuchukua hatua dhidi ya ukatili wa kijinsia unaofanyika katika mazingira ya kidijitali.