Highlands FM

Vyama vyataka haki na usawa kuelekea uchaguzi mdogo, Nonde

8 October 2026, 1:52 pm

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbeya Mjini na Uyole, Dkt. Laurence Kibona; Picha na Samwel Mpogole

Uchaguzi mdogo Nonde: Vyama vyataka haki na usawa katika mchakato wa uchaguzi, huku Tume ikiahidi kusimamia kwa mujibu wa sheria.
Je, maandalizi yakoje kuelekea Novemba 4? Fuatilia taarifa kamili hapa.

Na Samwel Mpogole

Viongozi wa vyama vya siasa jijini Mbeya wameitaka Tume ya Uchaguzi kuhakikisha uchaguzi mdogo wa Kata ya Nonde unasimamiwa kwa haki na usawa, wakisema hatua hiyo ni muhimu katika kulinda amani na kuzuia migogoro isiyo ya lazima.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Novemba 4 mwaka huu, kufuatia kifo cha aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo.

Viongozi hao wameitaka Tume ya Uchaguzi na wasimamizi wake kuhakikisha kila mgombea anapata haki sawa na mchakato mzima unafuata sheria na taratibu za uchaguzi.

Sauti za viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa Mbeya

Akijibu matakwa hayo, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbeya Mjini na Uyole, Dkt. Laurence Kibona, amesema wamejipanga kuhakikisha uchaguzi huo unasimamiwa kwa weledi na kwa kuzingatia kanuni na taratibu.

Sauti ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbeya Mjini na Uyole, Dkt. Laurence Kibona