Highlands FM
Highlands FM
12 November 2026, 12:02 pm

Je, watumishi wazembe na wasiozingatia maadili ya kazi Chunya wataendelea kuvumiliwa? Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Sozi Ngate, ametoa onyo kali na kuagiza hatua kuchukuliwa dhidi ya watumishi wanaokiuka miiko ya kazi,
Na Samwel Mpogole
Mkuu wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Mhe. Sozi Ngate, amewaagiza viongozi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha watumishi wanaokiuka maadili na miiko ya kazi, ikiwemo uzembe na utovu wa nidhamu, wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria na taratibu za utumishi wa umma.
Akizungumza katika Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Mkuu huyo wa Wilaya amesema Serikali haitavumilia uzembe, ubadhirifu wa rasilimali za umma na vitendo vinavyokwamisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Bw. Kelvin Shinshi, ameeleza msimamo wa Halmashauri katika kusimamia uwajibikaji na utekelezaji wa majukumu kwa watumishi.

Kwaupande wake Mbunge wa Jimbo la Lupa, Masache Njellu Kasaka, amezungumzia umuhimu wa usimamizi na uwajibikaji katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma zinazostahili.
Naye, Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Chunya, Francis Kisoma, amesisitiza umuhimu wa viongozi na watumishi wa umma kuzingatia misingi ya uadilifu na kupinga vitendo vya rushwa katika utekelezaji wa majukumu yao.
Aidha, Jeshi la Polisi Kupitia ka OCD wa wilaya hiyo Robert Milawi limehimiza ushirikiano kati ya viongozi, watumishi na wananchi katika kuzuia na kudhibiti vitendo vya uhalifu.
