Highlands FM

Wadau Kyela waungana kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana

26 November 2026, 3:03 pm

Watetezi wa haki za wanawake na wasichana pamoja na wadau kutoka asasi za kiraia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela {Picha Elizabeth Nyivambe}

Wadau wa asasi za kiraia wilayani Kyela wameungana kuhamasisha jamii kupinga ukatili wa kijinsia na kutetea haki za wanawake na wasichana kupitia utoaji wa elimu.

Na Mwanaisha Makumbuli

Katika kuadhimisha Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia, Tanzania imeungana na mataifa mengine duniani kuhamasisha jamii kuchukua hatua za pamoja katika kupinga na kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Kaulimbiu ya mwaka 2026 nchini Tanzania inasema “Tuungane Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto: Jenga Taifa Imara Lenye Haki na Usawa Kuelekea Dira 2050.”

Akizungumza wakati wa kufungua kikao cha watetezi wa haki za wanawake na wasichana kilichowakutanisha wadau kutoka asasi za kiraia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Elimisha, Bi. Debora Mwanyanje, amesema lengo ni kuunganisha nguvu za pamoja katika utetezi wa haki za wanawake na wasichana.

Sauti Mkurugenzi

Amesema ukatili wa kijinsia bado upo katika maeneo mbalimbali ya jamii, hivyo kila mmoja ana wajibu na haki ya kushiriki katika mapambano ya kukomesha vitendo hivyo.

Sauti Debora ukatili

Kwa upande wao, baadhi ya washiriki wa kikao hicho wamesema mkutano huo ni muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa wadau na kuongeza uelewa kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia.

Sauti Washiriki kyela
Watetezi wa haki za wanawake na wasichana pamoja na wadau kutoka asasi za kiraia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela

Wamesema wataendelea kutoa elimu kwa jamii na kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika kupinga ukatili wa kijinsia ili kulinda haki, usalama na utu wa wanawake na wasichana.