Highlands FM

RIKOLTO yawezesha wakulima kupata mikopo himilivu

24 November 2026, 10:33 am

Mratibu wa Programu kutoka Rikolto, Djalou Franko; Picha na Samwel Mpogole

Mikopo himilivu kufungua fursa kwa wakulima kuongeza uzalishaji na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Lakini je, matumizi sahihi ya maji yana nafasi gani katika kilimo endelevu?

Na Samwel Mpogole

Wakulima wanaotumia maji kwa shughuli za umwagiliaji wametakiwa kuwa na vibali halali vya matumizi ya maji ili kudhibiti matumizi ya rasilimali hiyo na kuhakikisha inadumu kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Bonde la Maji la Ziwa Rukwa, Emanuel Kisendi, katika kikao cha kuwasilisha na kuthibitisha matokeo ya utafiti kuhusu Mfumo wa Mikopo Himilivu, uliofanyiwa majaribio na Shirika la Rikolto kwa kushirikiana na Benki ya CRDB pamoja na TARI Ifakara.

Sauti ya Mkurugenzi wa Bonde la Maji la Ziwa Rukwa, Emanuel Kisendi.

Katika hatua nyingine, kikao hicho kimejadili Mfumo wa Mikopo Himilivu unaolenga kuwawezesha wakulima wadogo wa mpunga kupata mikopo na kutumia mbinu bora za kilimo zinazozingatia uhifadhi wa mazingira.

Mratibu wa Programu kutoka Rikolto, Djalou Franko, amesema mfumo huo unalenga kuongeza uwezo wa wakulima kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuwawezesha kupata huduma za kifedha zinazozingatia mahitaji yao.

Sauti ya Mratibu wa Programu kutoka Rikolto, Djalou Franko

Kwa upande wao, baadhi ya wakulima walionufaika na mfumo huo wameeleza namna ulivyowasaidia kuboresha shughuli zao za kilimo na kuongeza uzalishaji

Sauti ya baadhi ya wakulima walionufaika

Kwa ujumla, upatikanaji wa mikopo kwa wakulima na matumizi ya mbinu endelevu za kilimo, sambamba na utunzaji wa vyanzo vya maji, ni hatua muhimu katika kuimarisha uzalishaji na kulinda rasilimali za maji kwa vizazi vijavyo.

Baadhi ya washiriki wakiwa katika kundi wakijadili; Picha na Samwel Mpogole