Highlands FM

SHZRH Kuandaa bonanza la familia, huduma za afya bure

29 October 2026, 6:01 pm

Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (SHZRH) Dr Godlove Bwanji; Picha na Samwel Mpogole

SHZRH yaandaa bonanza la familia lenye huduma za afya BURE, michezo na burudani jijini Mbeya!
Jiandae kushiriki SHZRH Family Day 2026, tukio la afya, furaha na mshikamano wa familia.

Na Samwel Mpogole

Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (SHZRH) imeandaa bonanza maalumu la familia litakalotoa fursa kwa wananchi kupata huduma za afya bure, kushiriki michezo mbalimbali na kufurahia burudani, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha afya bora na kuimarisha mshikamano wa familia.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mkurugenzi wa Hospitali hiyi Dr Godlove Bwanji amesema Bonanza hilo linatarajiwa kufanyika Jumamosi, Oktoba 31, katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU), jijini Mbeya, kuanzia saa 12:30 asubuhi.

Wananchi watakaohudhuria watapata huduma za ushauri na uchunguzi wa afya bure, kushiriki mashindano mbalimbali ya michezo, burudani za watoto pamoja na kushiriki zoezi la uchangiaji wa damu salama.

Sauti ya Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Dr Godlove Bwanji

Aidha, bonanza hilo linatarajiwa kuwa jukwaa la kuwakutanisha wanafamilia katika mazingira ya furaha huku likitoa nafasi ya kuelimishana kuhusu umuhimu wa kujali afya, kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara na kuchangia damu ili kuokoa maisha.

Sauti ya katibu wa bonanza, dkt. Joyce komba na Mjumbe wa bonanza wakielezea hali halisi ya bonanza hilo

SHZRH imewaalika wananchi wa Mbeya na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi pamoja na familia zao kushiriki bonanza hilo, ambalo linaunganisha huduma za afya, michezo na burudani katika tukio moja.