Highlands FM
Highlands FM
22 October 2026, 10:47 am

Miezi sita bila mshahara! Wafanyakazi wa ushuru wa maegesho jijini Mbeya wafunguka kuhusu hali ngumu wanayopitia, huku mkurugenzi wa kampuni akieleza upande wake wa madai hayo.
Na Samwel Mpogole
Wafanyakazi wa kampuni ya Bezzu inayohusika na ukusanyaji wa ushuru wa maegesho ya magari katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya, wamelalamikia kutolipwa mishahara kwa zaidi ya miezi sita, hali wanayosema imewaweka katika wakati mgumu wa kumudu mahitaji yao ya kila siku.
Wafanyakazi hao, wanaokadiriwa kufikia 30, wamesema wameendelea kutekeleza majukumu yao licha ya changamoto za kifedha zinazowakabili, huku wakieleza kuwa ahadi za kulipwa mishahara yao zimekuwa hazitekelezeki.
Wamesema hali hiyo imewaathiri katika kutimiza majukumu yao ya kifamilia na mahitaji muhimu ya maisha, huku wakieleza hatua walizochukua.
Akizungumza kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa kampuni ya Bezzu, Benard Mwakyembe, amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo.