Highlands FM

Wanahabari wahimizwa kuimarisha afya ya akili

1 October 2026, 12:11 pm

Waandishi wa habari wakipokea mafunzo; Picha na Samwel Mpogole

Kutokana na changamoto za afya ya akili kuongezeka, waandishi wa habari wametakiwa kujenga uwezo wa kudhibiti na kuhimili hisia wanapotekeleza majukumu yao.Je, waandishi wanapaswa kuchukua hatua gani kujilinda?

Na Samwel Mpogole

Waandishi wa habari wametakiwa kujenga uwezo wa kudhibiti na kuhimili hisia wanapotekeleza majukumu yao, hasa wanapokutana na matukio yenye kushtua au kuathiri hisia, ili kujilinda dhidi ya changamoto za afya ya akili.

Ushauri huo umetolewa na Dkt. Raymond Mgeni kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya kitengo cha Afya na Magonjwa ya akili, wakati wa mafunzo yaliyolenga kuwajengea waandishi uelewa kuhusu usalama wao wanapotekeleza majukumu ya uandishi wa habari.

Sauti ya Dkt. Raymond Mgeni kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya

Baadhi ya waandishi walioshiriki mafunzo hayo wamesema wamepata uelewa zaidi kuhusu umuhimu wa kutambua, kudhibiti na kukabiliana na hisia zinazoweza kujitokeza wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kazi.

Sauti ya waandishi walioshiriki mafunzo

Mafunzo hayo pia yameweka msisitizo kuhusu umuhimu wa waandishi kuzingatia usalama wao wenyewe wanapotekeleza majukumu katika mazingira mbalimbali ya kazi, kama anavyoeleza Gabriel Mbwile, mkufunzi wa wakufunzi kutoka UTPC.

Sauti ya Gabriel Mbwile, mkufunzi wa wakufunzi kutoka UTPC