Highlands FM
Highlands FM
2 October 2026, 10:00 am

Wananchi wa Kata ya Mahongole, Mbarali mkoani Mbeya, wanatarajia kuondokana na changamoto ya usafiri wakati wa mvua baada ya ujenzi wa Daraja la Mlowo kufikia asilimia 85.
Na Samwel Mpogole
Wananchi wa Kata ya Mahongole, Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, wanatarajia kuondokana na changamoto ya usafiri, hasa wakati wa mvua, baada ya ujenzi wa Daraja la Mlowo kukamilika.
Mradi huo wa ujenzi wa Daraja la Mlowo lenye urefu wa mita 13.40 umezinduliwa na Mwenge wa Uhuru, ukiwa na lengo la kuboresha usafiri na mawasiliano kwa wananchi wa eneo hilo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Mwang’onda, amewataka wahandisi kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati.
Naye Meneja wa TARURA Mkoa wa Mbeya, Mhandisi William Lameck, amesema ujenzi wa daraja hilo umefikia asilimia 85 na kuwataka wananchi kulitunza baada ya kukamilika.
Kwa upande wao, wananchi wamesema kukamilika kwa daraja hilo kutarahisisha shughuli zao za kila siku.
