Highlands FM

Mafuriko Nzovwe nyumba 21 zabomoka, kaya 43 zakosa makazi

4 November 2026, 6:54 pm

Picha ya Jumanne Sagini Mkuu wa Mkoa wa Mbeya: Picha na Samwel Mpogole

Mafuriko Nzovwe, Mbeya: Nyumba 21 zimebomoka na kaya 43 kukosa makazi! Wananchi waomba msaada wa haraka huku Serikali na wadau wakichukua hatua kusaidia waathirika. Tazama taarifa kamili ujue kilichotokea.

Na Samwel Mpogole

Wanachi wa Kata ya Nzovwe jijini Mbeya wameiomba Serikali kuongeza kasi ya uchimbaji wa mitaro ya kupitisha maji ya mvua ili kudhibiti mafuriko yanayoendelea kuathiri eneo hilo, baada ya nyumba 21 kubomoka na kaya 43 kukosa makazi.

Baadhi ya waathirika wa mafuriko hayo wamesema wamepoteza makazi na mali zao, huku wakiiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kukabiliana na hali hiyo na kuzuia madhara zaidi.

Sauti ya baadhi ya wananchi waathirika,Ireni Hashimu na Joseph Mwakibete

Akizungumza baada ya kuwatembelea waathirika, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Jumanne Sagini amesema ujenzi wa barabara ya njia nne ni miongoni mwa changamoto zinazochangia kutokea kwa mafuriko katika eneo hilo, huku akiiagiza Halmashauri ya Jiji la Mbeya kuhakikisha waathirika wanapatiwa msaada wa kibinadamu.

Sauti ya Jumanne Sagini Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.

Wakati huo huo, wawakilishi wa wabunge wa Mbeya Mjini na Uyole wamefika katika eneo hilo kusaidia uratibu wa upatikanaji wa mahitaji muhimu kwa wananchi walioathirika na mafuriko hayo.

Sauti ya Hashimu Edward, Katibu wa Mbunge wa Mbeya Mjini na Joshua Edward, Afisa Habari, Taasisi ya Tulia Trust