Highlands FM

Uhaba wa wakalimani Mbeya waathiri huduma za afya kwa watu wenye uziwi.

1 October 2026, 12:16 pm

Mwenyekiti wa Chama Cha Viziwi Tanzania (Chavita) mkoa wa Mbeya, Tusajigwe Mwalwega [Picha Mwanaisha Makumbuli}

Pengo la mawasiliano kati ya wahudumu wa afya na watu wenye uziwi linaweza kufanya baadhi ya wagonjwa kushindwa kueleza kwa usahihi changamoto zao za kiafya na pia kupata maelekezo sahihi kuhusu matibabu.

Makala hii inaangazia uhaba wa wakalimani wa lugha ya alama Mbeya na athari zake katika upatikanaji wa huduma za afya kwa watu wenye ulemavu wa kusikia.

Na Mwanaisha Makumbuli

Uhaba wa wakalimani wa lugha ya alama mkoani Mbeya unatajwa kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu wa kusikia katika kupata huduma bora za afya.

Mkoani Mbeya kuna watu 12,000 wenye ulemavu wa kusikia, huku taarifa zikieleza kuwa angalau katika kituo kimoja cha kutolea huduma za afya hakuna mkalimani wa lugha ya alama, hali inayoweza kuongeza changamoto za kiafya na kijamii kwa kundi hilo.

Sauti Makala