Highlands FM

Sagini atoa siku 3 kwa bajaji kuondoka barabara kuu ya TANZAM Mbeya

11 November 2026, 7:18 pm

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Jumanne Sagini; Picha na Samwel Mpogole

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Jumanne Sagini, atoa siku tatu kwa bajaji kuondoka barabara kuu ya TANZAM! Je, ni barabara zipi zitatumika badala yake? Tazama taarifa hii kufahamu zaidi.

Na Samwel Mpogole

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Jumanne Sagini, amewapa siku tatu waendesha bajaji jijini Mbeya kuacha kutumia barabara kuu ya TANZAM na badala yake kutumia barabara za pembeni zilizoainishwa na Kamati ya Tathmini kuwa zinafaa kwa vyombo hivyo.

Hatua hiyo inafuatia kukamilika kwa tathmini ya upangaji wa matumizi ya barabara jijini Mbeya, iliyofanywa na kamati iliyoundwa kwa maelekezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Riziki Shemdoe.

Sauti ya Jumanne Sagini, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya

Awali, akiwasilisha ripoti ya tathmini hiyo, Mwenyekiti wa Kamati, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP Notker Kilewa, ameeeleza maeneo na barabara zilizobainika kufaa kwa matumizi ya bajaji.

Sauti ya SSP Notker Kilewa, Mwenyekiti wa Kamati ya Tathmini

Baadhi ya wadau waliohudhuria kikao hicho pia wametoa maoni yao kuhusu ripoti hiyo na maelekezo yaliyotolewa.

Sauti za baadhi ya wadau
SSP Notker Kilewa, Mwenyekiti wa Kamati ya Tathmini; Picha na Samwel Mpogole