Highlands FM

Dira ya taifa ya maendeleo yhitaji ushirikiano wa serikali na sekta binafsi

13 November 2026, 3:54 pm

Wadau wametakiwa kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi ili kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga kujenga uchumi shindani na jumuishi kupitia teknolojia, ubunifu na maarifa.

Na Lameck Chalres

Kuelekea utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga kujenga uchumi shindani na jumuishi unaotegemea maarifa, ubunifu na matumizi ya teknolojia, wadau wametakiwa kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi ili kufanikisha malengo hayo.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Rungwe, Ally  Kiumwa, wakati wa hafla ya tahmini ya ushirikiano wa wadau katika kuwezesha jamii kwenye masuala ya usimamizi wa mnyororo wa ugavi na usafirishaji kwa uchumi endelevu.

Sauti Ally

Aidha, ameliomba shirika hilo kuendelea kuwekeza katika fursa mbalimbali za maendeleo, hususan sekta ya kilimo na utalii, akibainisha kuwa Mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa mikoa yenye fursa kubwa na inayofanya vizuri katika sekta hizo.

Sauti Ally 2 fursa
Mkurugenzi wa Kühne Foundation Tanzania, Beatrice Millu

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kühne Foundation Tanzania, Beatrice Millu, amesema shirika hilo litaendelea kuunga mkono juhudi za maendeleo kwa kutoa fursa kwa wananchi wa mikoa ya Mbeya na Songwe kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali, ikiwemo miradi ya kilimo inayolenga kuwawezesha vijana kiuchumi.

Sauti Millu

Baadhi ya wanufaika wa miradi ya Kühne Foundation wameeleza kuridhishwa na mchango wa shirika hilo, wakisema mafunzo wanayopatiwa yamewasaidia kukuza uwezo wao, kutimiza ndoto zao na kujikwamua kiuchumi.

Sauti Wanufaika

Kühne Foundation Tanzania ni  shirika la kimataifa lisilo la faida la Kühne Foundation, lenye makao yake makuu nchini Uswisi. Shirika hilo linajihusisha na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo elimu ya usafirishaji na ugavi, maendeleo ya vijana, kilimo, afya na misaada ya kibinadamu.