Sibuka FM

zaidi ya bilion 10.8 kutatua changamoto ya maji hasa vijijini mkoani simiyu

30 October 2021, 7:59 am

Kwenye picha ni mkuu wa mkoa wa Simiyu David Kafulila akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani

Na mwandishi wetu Daniel Manyanga,Simiyu

Zaidi ya bilioni 10.8 zilizotolewa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu Hassan  zikiwemo zaidi ya  bilioni 8 za bajeti ya kawaida na zaidi ya  bilioni 2 ambazo ni fedha za uviko -19 mkoani Simiyu zinaenda kuondoa adha ya maji vijijini.

Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Simiyu David Kafulila akiwa kwenye kikao cha  baraza la madiwani wa halmashauri  ya wilaya ya  Itilima iliyopo mkoani hapo na kumpongeza  rais wa awamu ya sita Mhe,Samia Saluhu Hassan kwa kuzitumia fedha za uviko-19 kutekeleza miradi ya maji ambapo zingeenda kununua vifaa vya kukabiliana na ugonjwa wa corona .

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Simiyu David Kafulila akizungumza na madawani wa wilaya ya Itilima

Mbali na hilo amesema kuna mradi mkubwa wa maji kutoka ziwa victoria ambapo maji yatafikishwa  mkoa hapo kupitia bomba lenye urefu wa km 194  wenye thamani ya zaidi ya  shilingi bilioni 400 ambapo vijiji 244 vitanufaika mkoani hapo na kwenda kupunguza adha ya ukosefu wa maji hasa vijijini.

Mkuu wa mkoa wa Simiyu David Kafulila akizungumzia mradi mkubwa wa maji wa ziwa victoria mkoani hapo ambao utanufaisha vijiji 244

Kafulila amesema kuwa kwa kipindi cha miaka miwili upatikanaji wa maji ulikuwa asilimia 40.5 na sasa umefikia asilimia 67.5 sawa na ongezeko la asilimia 27 ambapo ameongeza  kuwa maji ni bidhaa na huduma muhimu pengine kuliko zote.

David Kafulila mkuu wa mkoa wa Simiyu kuongezeka kwa hali ya upatikani wa maji