Sibuka FM

Asilimia 40% ya vifo vya Watoto nchini vinatokana na watoto kuzaliwa Njiti.

26 September 2021, 11:15 am

Imeelezwa  kuwa  asilimia  Arobaini  ya  vifo  vya  Watoto  nchini  vinatokana   na  watoto  kuzaliwa  kabla   ya  siku  zao   (Njiti).

Hayo  yamesemwa  na  Mwenyekiti  wa  Kamati  ya  Kudumu   ya  Bunge  ya  Huduma  na  maendeleo  ya  Jamii  na  Mbunge  wa  Jimbo  la  Maswa  mashariki  Stanslaus  Nyongo  wakati   akipokea  vifaa  vya  kuhudumia  watoto  njiti  vilivyotolewa  na  Taasisi  ya  DORIS  MOLLEL   FOUNDATION  katika  Ukumbi  wa  Halmashauri  wilayani  Maswa, Mkoani   Simiyu.

Mh   Nyongo  amesema  kuwa  tatizo  la   watoto  njiti  linatatulika  endapo   watapewa  huduma  bora  na  kuondoa  unyanyapaa   na  mila  potofu  kwa  jamii   zikiamini  kuzaliwa  mtoto  njiti  kwenye  familia  ni  kupata  laana  na  mikosi inayoweza  kujitokeza  kwenye  familia  husika..

Sauti ya Stanslaus Nyongo

                 

Amesema  kuwa  mara  nyingi  kumekuwa  na  changamoto  kubwa  katika  kuwalea  watoto  wa  namna  hiyo  hali  ambayo  imekuwa  ikipelekea  baadhi  ya  akina  mama  kutoroka  hospitali  wakikwepa gharama  na  usumbufu  wa  namna  ya  kuwalea  watoto  hao..

Sauti ya Stanslaus Nyongo

               

Akikabidhi  Msaada   wa  vifaa  hivyo  vyenye  thamani  ya   zaidi  ya  Shilingi  Milioni  Hamsini   Mwanzilishi  na Mkurugenzi  wa  Tasisi  ya  Doris  Mollel  Foundation    Bi.  Doris  Mollel   ambaye  pia  yeye  alizaliwa  mtoto  njiti amesema  ameguswa  na   mahitaji  ya  watoto  wanaozaliwa  kabla  ya  wakati  huku  akielezea  ushuhuda  wake  wa  kuzaliwa  njiti…

Sauti ya Doris Mollel

                   

Aidha  mganga  mkuu wa  Wilaya  ya  Maswa  Dr   Adorat   Mpollo   amesema  kuwa  changamoto  hiyo  ipo ambapo  wastani  wa  watoto  Ishirini  na  tano  wanaozaliwa  kwa mwezi  katika Hospitali  ya Maswa kati  yao  nusu  ni  njitikati.

Sauti ya DMO Maswa Adorat Mpollo

                 

 Kwa  upande  wake   mwenyekiti  wa  Chama  cha  mapinduzi  wilaya  ya  Maswa  Mhandisi   Paul  Jidayi  amesema  kuwa  anawashukuru  sana  Taasisi  ya   Doris  Mollel  Foundation  kwa  kukuswa  na  kusaidia   watoto   wa  wilaya ya  Maswa  ambao  wamekuwa  wakipoteza  Maisha   kutokana  na  changamoto ya  kuzaliwa  njiti…

Sauti ya Paul Jidayi

                   

Baadhi  ya  wazazi  wa   watoto  njiti wamezungumza  na  Sibuka  fm  na  kuishukuru  Serikali  kwa   msaada  huo   kwani  wamekuwa  wakipata  changamoto  ya  kuwalea  na  kuwatunza  watoto  ambao  wamekuwa   wakizaliwa   kabla  ya  wakati….

Baadhi ya wazazi wenye Watoto njiti

        

Hapa chini ni Picha mbalimbali za mapokezi ya vifaa kwa ajili ya watoto Njiti

Kifaa cha kutunzia mtoto aliyezaliwa njiti
Kushoto ni DC MaswaAswege kaminyoge, katikati ni Slansaus Nyongo na mwishoni kulia ni Doris Mollel
Stanslaus Nyongo
Doris Mollel
Baadhi ya Watoto waliozaliwa njiti katika Picha ya pamoja