Sibuka FM

jeshi la polisi lawashikilia watano kwa mauaji simiyu

May 22, 2021, 8:58 pm

kwenye picha ni kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Simiyu ACP Richard Abwao

Jeshi la polisi mkoa wa Simiyu linawashikilia watu watano kwa tuhuma za  mauaji ya mtu mmoja.

Hayo yamesemwa na kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Simiyu ACP Richard Abwao wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari na kuongeza kuwa tukio hilo limetokea  Mei  20, 2021 mnamo majira ya  tisa usiku katika mtaa wa Kidurya kata ya Ntuzu wilayani Bariadi mkoani Simiyu.

” watuhumiwa walimuua mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Peter Ndwani ( 40) kabila Mmasai ambaye  alikuwa mlinzi kwenye nyumba ya John Sabu ambaye ni  mfanyabiashara wa mjini Bariadi na  aliuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani ambapo alipata majeraha kwenye paji la uso ” amesema Abwao

Aidha ACP Abwao ameongeza kuwa watu hao walivamia kwenye nyumba  hiyo kwaajili ya kuiba magunia ya alizeti ambapo ameongeza kuwa kulikuwa  na magunia 200 yenye thamani ya shilingi milioni 21.6.

Abwao amesema tayari jeshi la polisi linawashikilia watu watano kwaajili ya mahojiano na mara baada ya upelelezi kukamilika watafikisha jalada kwa mkuu wa mashitaka mkoa kwa hatua za kisheria zaidi ili wafikishwe mahakamani.

Sauti ya kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Simiyu ACP Richard Abwao