Sibuka FM

afariki dunia baada ya kudondokewa na matofali ya udongo

October 1, 2021, 1:31 pm

Mtoto wa miaka 03 Agnes Charles Masanja mkazi wa Kijiji cha Mwanzangamba kata ya Mwanyahima wilaya ya Meatu mkoani Simiyu amefariki dunia baada ya kudondokewa na matofali ya udongo katika nyumba yao.

Muonekano wa nyumba iliyopelekea kifo cha mtoto Agnes Charles Masanja miaka 3.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu ACP Richard Abwao amesema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 20:00 usiku mnamo tarehe 29/09/2021 baada ya Tembo wawili kubomoa nyumba aliyokuwa amelala mtoto huyo wakiwa wanatafuta chakula aina ya viazi vikavu {michembe}, mara baada ya tembo hao kugundua kuwa ndani ya nyumba hiyo kuna chakula wanachokihitaji kuwepo ndani ya nyumba hiyo.

Ameongeza kuwa mama wa mtoto huyo aitwaye Kulwa Jisanga miaka 26 ndiye alikuwa wa kwanza kumuokoa mtoto wake na kumkimbiza hospitali ya wilaya ya Meatu mara baada ya tembo hao kuondoka, ambapo hata hivyo mtoto huyo alikuwa tayari ameshafariki, awali mama huyo alikuwa amekimbia na  watoto wake wengine wawili waliokuwa nao nje ya nyumba.

Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na daktari Juma Makungu wa hospitali ya wilaya ya Meatu tarehe 30/09/2021 na kisha kukabidhiwa  kwa ndungu kwa ajili ya mazishi.

Sauti ya kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu Richrd Abwao akithibitisha taarifa hiyo ya kifo

Aidha Abwao amesema kuwa jeshi la polisi mkoa wa Simiyu linatoa wito kwa wananchi wote wanaoishi jirani na hifadhi kuendelea kuchukua tahadhari zinazotolewa na wataalamu ili kudhibiti tembo kuingia katika makazi ya wananchi.

Sauti ya RPC Simiyu Abwao akitoa rai wa wananchi kuchukua tahadhari kukabiliana na tembo