Sibuka FM

MALALAMIKO YA WACHIMBAJI WA MADINI, MGODI WA BULUMBAKA BARIADI YASHUGHULIKIWE.

April 16, 2021, 11:28 am

Uongozi wa mkoa wa Simiyu umetoa siku saba kwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi na Ofisi ya Madini Mkoa wa Simiyu kupitia malalamiko na hoja zote za wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba na wadau wengine katika mgodi wa dhahabu wa Bulambaka wilayani Bariadi na kuhakikisha shughuli za uchimbaji wa madini unafanyika kwa mujibu wa sheria.

Hayo yameelezwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga mara baada ya kuzungumza na wananchi hao waliofika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, ili kupata ufumbuzi wa malalamiko yao..

RAS-Simiyu Miriam Mmbaga

Nao baadhi ya wamiliki wa mashamba na wachimbaji wadogo ambao ni wananchi walioko eneo la mgodi la Bulumbaka wamesema kuwa kuna baadhi watu wenye mashamba hawajui namna leseni ilivyoapatikana maana hawakushirikishwa,

Aidha wachimbaji hao wameiomba serikali kuwatendea haki kwani wao ndio wamiliki wa mashamba hayo,