Karagwe FM

Kagera Network yawezesha matibabu kwa wenye ulemavu

26 November 2026, 23:40

Mratibu wa mradi wa “Wezesha Mtoto” Bi Ruth Hole. Picha na Jovinus Ezekiel

Baadhi ya mashirika yameendeleza ushirikiano katika mapambano dhidi ya ulemavu kwa vijana na watoto mkoani Kagera

Na Jovinus Ezekiel, Karagwe

Mtandao wa mashirika ya kuhudumia vijana na watoto wenye ulemavu mkoani Kagera, KAGERA NETWORK umefanikiwa kutoa huduma za matibabu na utengamao  kwa baadhi ya watoto wenye ulemavu katika jamii kupitia mradi wa Wezesha Mtoto.

Mtandao huo unaojumuisha mashirika matatu ya kuhudumia vijana na watoto wenye ulemavu ya CBIDO la wilayani Karagwe, MUDREO la Muleba na Caritas Rulenge la wilayani Ngara mkoani Kagera umewakutanisha wadau mbalimbali na kueleza mafanikio ya kutoa huduma za utengamao kwa kundi hilo kama alivyobainisha mratibu wa mradi wa Wezesha Watoto wa CBIDO Bi Ruth Hole

Sauti ya mratibu wa mradi wa “Wezesha Mtoto” Bi Ruth Hole
Martine Mwampamba kutoka shirika la Caritas Rulenge Ngara. Picha na Jovinus Ezekiel

Baadhi ya washiriki wameeleza kuwa mradi huo umekuwa na tija kubwa hasa kwa watoto wenye ulemavu hasa maeneo ya vijijini na kwamba umetoa elimu kuhusu ulemavu na kuleta matumaini kwa wanufaika wa matibabu

Sauti ya wawakilishi wa mashirika ya MUDREO na Caritas Rulenge Ngara
Viongozi wa Kagera Network. Picha na Jovinus Ezekiel