Karagwe FM

Watakaoathiriwa na El Nino watengewa maeneo salama Karagwe

16 October 2026, 15:55

Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Julius Laizer. Picha kwa hisani ya mtandao

Mkuu wa Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera Julius Laizer ameendeleza mikakati ya kuchukua tahadhari dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na mvua za El Nino wilayani humo.

Na Shabani Ngarama, Karagwe

Serikali wilayani Karagwe imetenga maeneo maalum kwa ajili ya wananchi watakaokumbwa na madhara ya mvua za El Nino licha ya kwamba maeneo hatarishi kwa wilaya hii siyo mengi

Akiongea na wandishi wa habari ofisini kwake Oktoba 16.2026 mkuu wa wilaya ya Karagwe Julius Laizer amewataka wananchi kutoa taarifa katika ofisi za vitongoji, vijiji na kata pindi watakapopata taarifa za viashiria vya maafa ya mvua kwenye maeneo yao ili kuiwezesha serikali kuchukua hatua za haraka

Amesema kuwa ni muhimu kwa wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi hasa mabondeni kuhama kwa hiari kabla ya kukumbwa na madhara ya mvua za El Nino ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Karagwe Julius Laizer

Pia Laizer ameitaka idara ya afya kwa kushirikiana wasimamizi wa vyanzo vya maji wilaya ya Karagwe kuhakikisha mazingira yanakuwa salama ikiwa ni pamoja na kuzuia wananchi wasifungulie chemba za vyoo ili kuepuka magonjwa ya mlipuko huku akisisitiza kuwa maeneo salama wametengwa kwa ajili ya huduma kwa watakakumbwa na madhara ya El Nino

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Karagwe Julius Laizer

Hata hivyo amewatoa hofu wananchi akisema kuwa si lazima madhara yatokee maeneo mengi pindi mvua zitakaponyesha kwa sababu jiografia inatofautiana kutokana na maeneo yanayopata mvua nyingi na yenye mvua za wastani. Amewaasa madereva kuchukua tahadhari pindi watakapokutana na maji mengi barabarani ili kuepuka ajali ikiwa barabara zitaathiriwa na mvua hizo. Mwiho amewaasa watendaji wa shirika la umeme TANESCO na umma kwa ujumla kukata miti hatarishi kando ya miundombinu ya umeme na makazi ya watu ili kuzuia miti hiyo kuhatarisha maisha ya wananchi nyakati za mvua zitakazoambatana na upepo.