Karagwe FM

Kamati ya siasa yaridhishwa utekelezaji Ilani ya CCM Karagwe

7 December 2023, 10:21 pm

Wajumbe wa kamati ya Siasa ya chama cha mapinduzi CCM wilaya Karagwe baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la utawala la halmashauri ya wilaya Karagwe linaloendelea : Eliud Henry

Na Eliud Henry

Karagwe

Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya Karagwe imeridhishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleleo na kuagiza kurekebisha kasoro ndogondogo ili kuhakikisha irani ya chama hicho ya mwaka 2020/2025 inatekelezwa ipasavyo.

Hayo yamebainika katika ziara ya kamati ya siasa ya CCM wilaya Karagwe ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa ilani ya chama hicho ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya Karagwe Ndg. Paschal Rwamgata iliyofanyika Disemba saba mwaka huu.

Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa na kamati hiyo ni pamoja na ujenzi wa bweni la kisasa la wasichana pamoja vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari ya Kawela iliyopo katika kata ya bweranyange ujenzi Ambapo mwenyekiti wa CCM wilaya ya Karagwe ameonshwa kuridhishwa na ujenzi huo.

Mwonekano wa Bweni jipya la wavulana lililojengwa katika shule ya Sekondari Nyakasimbi iliyopo katika kata ya Nyakasimbi wilayani Karagwe picha na: Eliud Henry
Sauti ya Mwenyekiti wa CCM wilaya Karagwe ndg Paschal Rwamgata: Eliud Henry

Aidha kamati hiyo imetembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa mabweni pamoja na vumba viwili vya marasa katika shule ya sekondari Nyakasimbi, ujenzi wa shule mpya ya Omurushaka iliyopo katika kata ya Bugene pamoja na ujenzi wa Jengo jipya la utawala la halmashauri ya wilaya Karagwe litakalogharimu zaidi ya sh. Bil.3.7

Jengo la utawala la halmashauri ya wilaya Karagwe linaloendelea kujengwa litakalogharimu zaidi ya sh. Bil.3.7: Eliud Henry

Walles Mashanda ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Karagwe hapa anaonyesha kufurahishwa na utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi.

Sauti ya Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Karagwe Walles Mashanda

Kwa upande wake mkuu wa wilaya Karagwe Julius kalanga laiser amewataka wasimamizi wa miradi hiyo kufanya kazi kwa uadirifu wa hali ya juu.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya Karagwe Julius kalanga Laiser