Karagwe FM

Anatropia Theonest aendelea kutatua changamoto za wananchi

27 October 2023, 10:04 pm

Na Jovinus Ezekiel

Jumla ya mifuko 40 ya saruji imetolewa na mbunge wa viti maalum mkoani Kagera Anatropia Theonest kwa lengo la kuwezesha ujenzi wa miradi ya zahanati ya Milambi na shule  shikizi ya msingi Omukiyonza inayotekelezwa katika kata ya Nyaruzumbula wilayani Kyerwa.

Akizungumuza na mwandishi wa Radio Karagwe 91.4 FM katibu wa mbunge wa viti maalum mkoa wa Kagera Evodius Katalama amesema kuwa lengo la mbunge wa viti maalum mkoa wa kagera Anatropia Theonest kutoa mifuko hiyo 40 ya saruji ni baada ya kufika katika kata ya Nyaruzumbula wilayani Kyerw a kwenye kipindi cha mwezi wa nane ili kubaini changamoto za wananchi na kuhaidi kutoa mifuko 40 ya saruji ili kuunga mkoni jitihada za ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Milambi na ujenzi wa shule ya msingi Shikizi katika kijiji cha Omukiyonza katani humo.

Amesema kuwa mifuko hiyo ya saruji ambayo mpaka sasa imekwishatolewa itasaidia kuendeleza ujenzi wa miradi hiyo kwani mh Anatropia amekuwa na utaratibu wa kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya jimbo la Kyerwa ambayo imejikita kwenye sekta ya elimu, afya na miundombinu.

Mahojiano kati ya Jovinus Ezekiel na Katibu wa mbunge wa viti maalum mkoa Kagera Bw. Evodius Katalama

Hata hivyo Bw, Katalama amewataka wananchi wa jimbo la Kyerwa kuendelea kushirikiana kwa pamoja na mbunge wa viti maalum mkoa wa Kagera Anatropia Theonest bila kujali itikadi za vyama vyao vya siasa kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo la Kyerwa.