Karagwe FM

Madiwani Missenyi walalamikia kasi ndogo ujenzi wa VETA

22 April 2024, 5:00 pm

Baadhi ya madiwani (kamati ya fedha, uchumi na mipango) halmashauri ya Missenyi wakiwa na mkurugenzi wa halmashauri hiyo John Paul Wanga (mwenye notebook na karatasi kulia).

Picha na Respicius John

Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi mkoani Kagera ni moja katika ya mabaraza yaliyo makini kwa kufuatilia matumizi ya fedha zinazopitishwa na baraza hilo kwa ajili ya miradi ya maendeleo

Na Respicius John

Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi mkoani Kagera wamelalamikia kasi ndogo ya ujenzi wa chuo cha mafunzo ya ufundi stadi VETA Buyango kinachonjwa na serikali kuu kwa gharama ya shilingi milioni 350 katika kata ya Buyango wilayani humo.

Katika ziara ya kamati ya fedha, utawala na mipango ya halmashauri ya wilaya hiyo madiwani walioambatana na wataalam wa halmashauri na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Missenyi wamesema kuwa hawajaridhishwa na kasi ujenzi wa chuo cha VETA Buyango ambapo diwani wa kata ya Bwanjai bw.Focas Rwegasira alibaini kasoro kadhaa katika mradi huo huo.

Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi

Jengo la chuo cha VETA Buyango wilaya ya Missenyi.

Picha na Respicius John

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Missenyi bw. John Paul Wanga amekiri kuwa kamati ya fedha, uchumi na mipango haijaridhishwa na ujenzi kutokana na kasoro mbalimbali walizozibaini ikiwemo kukiuka baadhi ya mashariti ya ubora katika vifaa vya ujenzi na usimamizi.

Sauti ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi John Paul Wanga

Mwisho