Karagwe FM

Mtendaji wa kijiji atumbuliwa na Madiwani

2 August 2021, 9:34 am

Baraza la madiwani wilaya ya Karagwe mkoani Kagera limemfukuza kazi mtendaji wa kijiji cha Omkakajinja kata ya Rugela kwa tuhuma za kuuza Ardhi ya kijiji hekari 30.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Karagwe na Diwani kata ya Nyaishozi, Mhe. Wallace Mashanda

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Karagwe na Diwani kata ya Nyaishozi, Mhe. Wallace Mashanda Amesema kuwa uamuzi huo umechukuliwa July 28 mwaka huu na baraza hilo baada ya kujilidhisha pasipo shaka kuwa mtendaji huyo ameuza Ardhi hiyo na kughushi nyaraka mbalimbali bila kufuata utaratibu na sheria.

Wallace Mashanda – M/Kiti Halmashauri ya wilaya Karagwe