Karagwe FM

Lishe duni chanzo cha ongezeko la watoto njiti Karagwe

10 May 2024, 10:50 am

Mganga mkuu wa wilaya ya Karagwe Dkt Agnes Mwaifuge (katikati) akisisitiza jambo. Picha na Ospicia Didace.

Pamoja na mkoa wa Kagera kuwa na wingi wa vyakula, ni mmoja kati ya mikoa inayotajwa kuwa na utapiamlo pamoja na udumavu kutoka na wananchi kutozingatia matumizi sahihi ya vyakula hivyo.

Na Ospicia Didace

Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe mkoani Kagera Dkt.Agness Mwaifuge amewataka akina mama wajawazito kula vyakula vyenye lishe pamoja na kuhudhuria kliniki kwa wakati jambo litakalosaidia kukabiliana na changamoto ya akina mama hao kujifungua watoto njiti

Hayo yalisemwa na mganga mkuu wa wilaya ya Karagwe Dkt. Agness Mwaifuge ambaye ni katibu wa  kikao cha kamati ya lishe kilichofanyika katika ukumbi wa Angaza mjini Kayanga wilayani Karagwe hivi karibuni akisema kuwa wilaya ya Karagwe kuna ongezeko la kuzaliwa watoto njiti huku akitaja changamoto kubwa kuwa ni ukosefu wa lishe kwa akina mama waja wazito.

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya lishe wilaya ya Karagwe.

Picha na Ospicia Didace

Dkt Mwaifuge amewataka wadau wa lishe kushirikiana kwa pamoja katika kutoa elimu kwa jamii juu ya mama mjamzito kupata mlo kamili  pamoja na kupunguziwa kazi za nyumbani.

Sauti ya Dkt Agnes Mwaifuge.

Naye mratibu wa lishe wilaya ya Karagwe bi Lustica Mgumba amezitaja changamoto zinazosababisha kuzaliwa kwa watoto njiti, midomo sungurua, mgongo wazi pamoja na magonjwa mengine kuwa ni pamoja na akina mama waja wazito kutotumia vidonge vya folic acid wakiamini kuwa vinaongeza damu wakati wa kujifungua jambo ambalo sio sahihi.

Sauti ya mratibu wa lishe wilaya ya Karagwe Bi Lustica Mgumba.

Akitoa maoni katika kikao hicho sheikh wa BAKWATA  wilaya ya Karagwe Alhaj Nassib Abdul Abdallah amempongeza mratibu wa lishe kwa kusimamia vizuri idara hiyo kwa kutoa elimu katika ngazi ya kijiji ambapo pia amewahimiza wadau wa lishe kuendelea kutimiza wajibu wao ili kusaidia jamii kuzingatia lishe kwa usahihi

Sauti ya sheikh wa BAKWATA  wilaya ya Karagwe,Alhaj Nassib Abdul Abdallah .