Karagwe FM

Askofu Bagonza ataja kundi la wabakaji Karagwe

23 April 2024, 9:23 pm

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe Mch.Dk Benson Bagonza. Picha na Eliud Henry

Kumekuwa na wimbi kubwa la vitendo vya ubakaji wa watoto wilayani Karagwe mkoani Kagera ambapo ndani ya kipindi kifupi kwa mujibu wa ofisi za ustawi wa jamii hadi Machi 4, 2024 zimeripotiwa kesi 16 za ubakaji na zote zikihusu watoto wenye umri chini ya miaka 13.

Na Eliud Henry

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe Mch. Dkt. Benson Kalikawe Bagonza, kwa mara ya kwanza ametaja chanzo cha vitendo vya ubakaji kwa watoto wilayani Karagwe mkoani Kagera akisema kuwa ongezeko la ubakaji limetokana na kuongezeka kwa vitendo vya rushwa na imani za kishirikina

Akiongea katika mahojiano maalum na Radio Karagwe Aprili 23, 2024 nyumbani kwake Bomani Kayanga Askofu Bagonza amesema watu waliopewa dhamana ya kusimamia sheria za kulinda haki za watoto wanaposhindwa kufanya hivyo wanageuka wabakaji hata kwa watoto ambao bado hawajazaliwa.

Sauti ya Askofu Bagonza