Karagwe FM

DAS Karagwe akabidhi misaada ya Rais Samia kwa makundi maalum

16 April 2024, 8:10 am

Imekuwa desturi ya viongozi wakuu  wa serikali na mashirika ya umma na binafsi kutoa zawadi za sikukuu za kidini kama Krismas, Mwaka  mpya, Pasaka na hata Eid El fitri na eid el addha kwa ajili ya kuwezesha makundi maalum kufurahia sikukuu kama watu wengine

Katibu tawala wilaya ya Karagwe (aliyevaa kanzu na kofia kulia) Rasul Eliud Shandala akikabidhi msaada wa vyakula na vinywaji kwa mkurugenzi wa shirika lisilokuwa la kiserikali TOSO bi Aines Samweli (anayetabasamu kushoto akishikilia kamba ya mbuzi) linalohuduma watu wenye mahitaji maalum. Picha na: Thomas Ntobi-Afisa habari wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe

Na Ospicia Didace

Vijana na watoto wanaosoma ufundi katika kituo cha watoto yatima TOSO katika kata ya Kayanga wilayani Karagwe wamenufaika na msaada wa mahitaji ya sikukuu ya eid el fitri kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kupitia ofisiya mkuu wa wilaya ya Karagwe.

Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Rais Samia hivi karibuni katibu tawala wa wilaya ya Karagwe bw. Rasul Eliud Shandala aliyemwakilisha mkuu wa wilaya ya Karagwe bw.Julius Laizer akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Karagwe Dr. Amon David Mkoga na baadhi ya wataalamu wa halmashauri hiyo amewataka wazazi kutowabagua na kuwanyanyasa watoto wenye ulemavu na badala yake wawape mahitaji ya msingi sawa na watoto wengine

Sauti ya katibu tawala wilaya ya Karagwe Rasul Eliud Shandala

Kwa upande wake mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima TOSO wilaya ya Karagwe AINES Samwel amemshuru Rais Samia kwa msaada huo na kutoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kuiga mfano wa Rais wa kula sikukuu na wenye mahitaji wakiwemo yatima

Bw.Shandala aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Julius Kalanga Laiser ambaye yupo kwenye majukum mengine ya kikazi na kukabidhi misaada mbalimbali ikiwemo Mbuzi mmoja, Mchele, Sukari, Mafuta ya kupikia, Chumvi, Vinywaji, Maharage pamoja na Sabuni za kufulia na kuogea

Wanafunzi na mkurgenzi wao bi Aines Samweli wakifurahia zawadi zilizotolewa kwa ajili ya sikukuu

Picha na Thomas Ntobi-Afisa habari wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe