Karagwe FM

Opareshen peperusha bendera ilivyofana Kata Kayanga – Karagwe

20 November 2023, 8:10 pm

Katibu wa itikadi na uenezi CCM wilaya ya Karagwe Mwl. Mugisha Thimotheo kulia akiwa na viongozi wa CCM Kata Kayanga.

Ziara ya oparesheni peperusha bendendera imelenga kuhamasisha masuala ya utawala bora, kuhamasisha kusajiliwa kwa njia ya elektronik, kuhamasisha uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2025 pamoja na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo.

Na Ospicia Didace

Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM pamoja na  viongozi wa serikali wametakiwa kuwahudumia wananchi kwa weredi na kuepuka vitendo vya rushwa vinavyoweza kupelekea unyanyasaji wa wananchi.

Wito huo umetolewa na Katibu wa itikadi na uenezi CCM wilaya ya Karagwe Mwl. Mugisha Thimotheo akiwa anaendelea na Operation ya peperusha Bendera katika kata ya Kayanga Novemba 19 2023.

Sauti ya Katibu wa itikadi na uenezi CCM wilaya ya Karagwe Mwl. Mugisha Thimotheo

Mwenezi akiwa amebaki na kata moja kumaliza oparation ya kata zote amesema kuwa amebaini baadhi ya wenyeviti wa vitongoji na vijiji kutoa huduma mbaya kwa wananchi kwa kutanguliza masilahi mbele huku akisema kuwa msimamo wa chama cha mapinduzi ni kuwahudumia wananchi bure.

Moja ya malengo ya oparation hiyo ikiwa ni kuhamasisha wananchi kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa ,mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya Karagwe amesema malengo ya chama chochote ni kushika dola hivyo Siraha ya kufanikisha hilo ni ushirikiano undugu na umoja miongoni mwa Wanachama na kuondoa fitina.

Mwenyekiti wa CCM kata kayanga Edson Chakatuka na katibu wa UWT Masitidia Rushambila wameeleza namna bendera hiyo itaamsha hari ya wana CCM.

Sauti za Katibu wa UWT Masitidia Rushambila na Mwenyekiti wa CCM kata kayanga Edson Chakatuka

Ziara ya oparation peperusha Bendendera imelenga kuhamasisha masuala ya utawala bora,kuhamasisha kusajiliwa kwa njia ya electronic,kuhamasisha uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2025 pamoja na Kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo.