Karagwe FM

Kitendawili kizito chateguliwa Bushenya!

6 November 2021, 11:35 am

Wananchi wanaoishi katika msitu wa Bushenya kata ya Nsunga wilaya ya Missenyi wametakiwa kuhama katika maeneo hayo kabla ya serikali kuanza operesheni ya kuwaondoa.

Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya Misenyi Kanali Wilson Sakulo kupitia kikao cha Baraza la madiwani wilayani humo kilichoketi kujadili taarifa mbalimbali za kimaendeleo Nov 4 na 5 mwaka huu ikiwa ni robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Baadhi ya Madiwani – wilaya ya Misenyi.

Awali kupitia kikao hicho,Wawakilishi wa wananchi ambao ni madiwani wa kata zilizoko wilayani Misenyi wametoa maoni yao baada ya kupokea taarifa ya kamati maalumu iliyoundwa kufuatilia msitu huo iliyowasilishwa na Bwana James Matekere ambaye ni Afisa misitu wilaya Misenyi.

Bwana Amudi Migeyo ni diwani kata Bugandika amesema swala la msitu wa Bushenya siyo la kufumbia macho na akaungwa mkono na madiwani wenzake.

Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya wilaya Misenyi

Baada ya madiwani hao kutoa maoni yao,Mkuu wa wilaya hiyo Kanali Wilsoni Sakulo akaeleza msimamo wa serikali juu ya mikakati na maamuzi yaliyowekwa na wilaya hiyo kwaajili ya kunusuru uharibifu wa uoto wa asili katika msitu huo.

DC – WILSON SAKULO

Misitu ni uhai na sio tu kwa binadamu na mazingira bali pia kwa asilimia 80 ya viumbe vyote vya porini, hivyo kutumia vyema na kuilinda ni kwa maslahi ya watu wote.