Karagwe FM

Wapewa mbinu mpya ili kupata Utajiri.

26 May 2021, 8:05 pm

Wanawake wilayani Karagwe wametakiwa kujikumbusha mbinu za masoko ili kuanzisha,kudumisha na kukuza biashara katika ngazi za kikanda na kimataifa.

Jeniffar Bashungwa – Mkurugenzi wa Alaska Jamii.

Ameyasema hayo Mke wa Mbunge wa jimbo la Karagwe ambaye ni mkurugenzi wa Alaska Jamii Bi Jeniffar Bashungwa wakati akiongea na wanawake viongozi wa vikundi katika tarafa ya Kituntu kupitia warsha ya ujasiriamali iliyofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoriki Parokia ya Rwambaizi.

Bi Jeniffar amesema,lengo la mafunzo hayo ni kutoa fursa kwa wanawake wanaofanya na wanaokusudia kufanya biashara mipakani kwa kuzingatia jinsia,Haki na Fursa sawa baina ya wanawake na wanaume.

Baadhi ya Washiriki wa warsha hiyo kutoka (W) Karagwe

Naye katibu wa Mbunge wa Jimbo la Karagwe Ivvo Ndisanye kwa niaba ya Mbunge amesema kuwa mafunzo hayo yaliyotolewa ni moja ya ahadi zilizotolewa na Mbunge wakati wa Kampeini zake za kuwania ubunge.

Mafunzo hayo yametolewa na Taasisi ya Alaska Jamii kwa kushirikiana na Chama cha wanawake Wajasiriamali Tanzania TWCC,,Trade Mark East Afrika,Halmashauri ya wilaya Karagwe kwakushirikiana na ofisi ya Mbunge Karagwe