CWT Missenyi
Karagwe FM

200 wapewa mbinu ili kutimiza ndoto zao.

9 November 2021, 11:52 am

Imeelezwa kuwa suala la vijana kutumiwa na baadhi ya vikundi vya watu kuanzisha vurugu mbalimbali inaweza kuwa chanzo kikubwa cha kuhatarisha amani ya nchi na kuharibu ndoto za vijana kufikia malengo yao.

Akizungumuza novemba 7 mwaka huu wakati wa kufunga kongamano la vijana zaidi ya 200 kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na visiwani Zanzibar waliokutanishwa katika ukumbi wa chuo cha Jocuko kata ya Nyakato wilayani Bukoba kwa lengo la kuwezeshwa juu ya mafunzo ya kuondokana na utegemezi na kutumia fursa zinazowazunguka ili kujinufaisha kiuchumi yaliyoratibiwa na shirika la shina Tanzania,Mgeni rasmi katika kongamano hilo Rasitus Kasimu Dhahabu afisa tarafa ya Bugabo kwaniaba ya mkuu wa wilaya ya Bukoba  amesema kuwa  ili vijana waweze kufikia ndoto zao inabidi wajiuepushe na masuala ya kuanzisha vurugu kwani vitendo hivyo vinaweza kuathiri ndoto zao na kuaribu amani ya nchi.

Rasitus Kasimu Dhahabu

Nao vijana walioshiriki konagamano hilo akiwemo Mwanahamisi Badru kutoka Zanzibar Nelson Mtawala kutoka wilaya ya Bukoba vijijini na Renatus Vicent kutoka mkoani Dodoma wameshukuru shirika la shina Tanzania kwa kuwapatia mafunzo ya kiutawala na uongozi katika siasa kwani mafunzo hayo yatawawezesha kujiepusha na vitendo vyenye viashiria vya kuwaingiza katika vurugu.

Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo.

Hata hivyo shirika la shina Tanzania linalofanya kazi zake za kuhudumia makundi mbalimbali ya wanawake, watoto wasio na uwezo kuwasomesha pamoja na wazee kuwahudumia wazee  katika mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na visiwani Zanzibar limetambua mchango wa wadau wanaoendelea kushirikiana na vizuri na shirika hilo ikiwemo redio karagwe kwa kuwatunuku vyeti vya kutambua mchango wao.

Mgeni Rasmi & washiriki