Karagwe FM

WASTAAFU MILANGO YA KUSHIRIKIANA NA HALMASHAURI IPO WAZI~DED MULEBA

27 January 2022, 9:33 pm

Na Lucia Binamungu, Muleba

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Ndugu Elias Kayandabila amekutana na kufanya mazungumzo na Mstaafu Ndugu Angelo Paul Rutainurwa tarehe 27.01.2022, mkazi wa Kata ya Nshamba ambaye kwa sasa anajishugulisha na masuala ya ushauri katika sekta za uongozi.

Ndugu Rutainurwa ni mbobezi katika kushauri viongozi waandamizi wa Serikali, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Biashara na vikundi vya kijamii juu ya kutekeleza mipango kazi yao na kupata matokeo chanya, sahihi na endelevu. Hivyo ameamua kuendeleza ujuzi wake kwa kuitumikia jamii yake huku akimueleza Mkurugenzi kuwa yupo tayari kushirikiana naye katika kuwajengea uwezo watumishi juu ya masuala ya uongozi katika sehemu zao za kazi.

Mkurugenzi Mtendaji amempokea na kumuahidi kumpa ushirikiano na kumtumia kwa ajili ya kuwajengea uwezo watumishi. Pia amemshukuru kwa wazo lake la kutaka kushirikiana na Halmashauri ili kuboresha utendaji kazi.

Amempongeza kwa kuona umuhimu wa kustaafu na kurudi kuishi nyumbani kwani ni wastaafu wachache wanaostaafu na kurudi kwao kisha kujitoa kuendelea kuutumia ujuzi walionao kwa manufaa ya jamii yake.

Aidha, Mkurugenzi ametoa wito kwa wastaafu wengine ambao ni wazawa wa Muleba kufika na kushirikiana na Halmashauri katika maeneo mbalimbali,