Karagwe FM

Madereva walia na ubovu wa stendi.

28 April 2021, 1:49 pm

Mwonekano wa stendi wakati wa Masika

Madereva wa Tax katika stendi ya Kayanga wilaya ya Karagwe Mkoa Kagera wameiomba serikali wilayani humo kufanya marekebisho ya stendi kutokana na stendi hiyo kujaa maji na tope wakati wa masika.

Sauti za baadhi ya Madereva Tax

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Karagwe bwana Wallece Mashanda amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kwamba taratibu za kuikarabati zinaendelea  hivyo amewaomba madereva tax kuwa wavumilvu.

Mh.Wallace Mashanda Mwenyekiti wa Halmashauri (w) Karagwe