Karagwe FM

Dr.Samia aombwa kusimama na watoto wa kike

29 April 2024, 9:39 pm

Msajili wa bodi ya usajili wa wahandisi (ERB) mhandisi Bernard Kavish akizungumza na walimu katika shule ya sekondari Kagera River. Picha na Devid Geofrey

Haikuwa rahisi kwa vijana wa kike kupenya na kufaulu vizuri katika taaluma kama walivyo vijana wa kiume hapa nchini Tanzania na watu wengi waliamini hivyo huko nyuma. Jambo hili pia lilisababisha wanafunzi wa kike kusita kuchagua kusoma masomo ya sayansi.

Na Devid Geofrey:

Wazazi na walezi wilayani Karagwe wametakiwa kuwasomesha watoto wa kike ili kuongeza idadi ya wahandisi wa kike na kukabiliana na uhitaji uliopo nchini.

Wito huo umetolewa na msajili wa bodi ya usajili wa wahandisi (ERB) mhandisi Bernard Kavish alipotembelea shule ya msingi Ahakishaka,shule ya sekondari ya Nyabiyonza pamoja na shule ya sayansi ya wasichana Kagera River zilizoko wilayani Karagwe April 29 2024.

Kwa Upande wake mhandisi Ester Christopher makamu mwenyekiti wa taasisi ya wahandisi Tanzania kitengo cha wanawake amesema kuwa wameamua kutembelea shule hizo ili kuwapa motisha watoto wa kike waweze kuongeza bidii katika masomo yao na kufikia ndoto walizonazo huku akieleza uwepo wa idadi ndogo ya wahandisi wa kike nchini.

Sauti ya mhandisi Ester Christopher

Mwalimu Johnbosko Bahati Paul ni kaimu afisa elimu sekondari halmashauri ya wilaya Karagwe amesema ujio wa wahandisi hao umeongeza hamasa kwa wanafunzi wa kike wilayani Karagwe kusoma masomo ya sayansi na akamshukuru mbunge wa jimbo la Karagwe na waziri wa ujenzi Innocent Bashungwa kwakupambana na kuhakikisha shule za sekondari wilayani Karagwe zinapata miundombinu yenye kuwafanya wanafunzi wa sekondari kusoma kwenye mazingira mazuri.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sayansi ya wasichana Kagera River iliyoko wilaya ya Karagwe. Picha na Devid Geofrey

Mwalimu Felister Francis ni mkuu wa shule ya sayansi ya wasichana Kagera River iliyoko katika kata ya Kanoni wilaya Karagwe ameushukuru uongozi wa serikali ya rais Dr.Samia kwakuwapa pesa zaidi ya shilingi bilioni nne ambazo zimetumika vyema kutekeleza miundombinu ya shule hiyo.

Mwalimu Felister Francis ni mkuu wa shule ya sayansi ya wasichana Kagera River